Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Al-Hashr — Ayah 16

59:16
كَمَثَلِ ٱلشَّيۡطَٰنِ إِذۡ قَالَ لِلۡإِنسَٰنِ ٱكۡفُرۡ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّي بَرِيٓءٞ مِّنكَ إِنِّيٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلۡعَٰلَمِينَ ١٦
Ni kama mfano wa Shetani anapo mwambia mtu: Kufuru. Na akikufuru humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.1
Footnotes
  • [1] Mfano wa wanaafiki kuwashawishi Banu Nnadhir wamuasi Mtume wa Mwenyezi ni kama mfano wa Shetani pale anapo mghuri mtu aiache Imani, akamwambia: Kufuru! Na alipo kufuru akasema: Mimi niko mbali nawe, kwani mimi ninamkhofu Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.