Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Al-Mumtahanah — Ayah 3

60:3
لَن تَنفَعَكُمۡ أَرۡحَامُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡۚ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَفۡصِلُ بَيۡنَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ ٣
Hawatakufaeni jamaa zenu, wala watoto wenu Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu atapambanua baina yenu, na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.1
Footnotes
  • [1] Hawatakufaeni kitu jamaa zenu wala watoto wenu mlio wafanya kuwa ni marafiki, na hali wao ni adui wa Mwenyezi Mungu na adui zenu. Katika Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atakutengeni mbali mbali. Atawatia maadui zake Motoni na marafiki zake Peponi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote myatendayo.