Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Al-Jumu'ah — Ayah 1

62:1
يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ ٱلۡمَلِكِ ٱلۡقُدُّوسِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ ١
Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme, Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.1
Footnotes
  • [1] Vitu vyote viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi vinamsabihi na kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila kisicho kuwa laiki, Yeye ndiye Mfalme wa kila kitu, Mwenye kuendesha atakavyo bila ya mpinzani, Mwenye kutakasika kwa ukamilifu na kila cha upungufu, Mwenye kushinda kila kitu, Mwenye hikima ya kufika mwisho.