Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Al-Hujurat — Ayah 13

49:13
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقۡنَٰكُم مِّن ذَكَرٖ وَأُنثَىٰ وَجَعَلۡنَٰكُمۡ شُعُوبٗا وَقَبَآئِلَ لِتَعَارَفُوٓاْۚ إِنَّ أَكۡرَمَكُمۡ عِندَ ٱللَّهِ أَتۡقَىٰكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٞ ١٣
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.1
Footnotes
  • [1] Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni nyinyi sawa sawa kutokana na asli moja, ya Adamu na Hawa. Na tukakufanyeni mkawa wengi kwa mataifa makubwa na makabila mengi, ili kutimie kujuana na kuawiniana baina yenu, sio kubaguana. Na hakika mwenye cheo cha juu miongoni mwenu kwa Mwenyezi Mungu duniani na Akhera ni yule anaye mcha Yeye zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa kuvijua, ni Mwenye khabari za dogo na kubwa la kila jambo.