Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Al-Hujurat — Ayah 6

49:6
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن جَآءَكُمۡ فَاسِقُۢ بِنَبَإٖ فَتَبَيَّنُوٓاْ أَن تُصِيبُواْ قَوۡمَۢا بِجَهَٰلَةٖ فَتُصۡبِحُواْ عَلَىٰ مَا فَعَلۡتُمۡ نَٰدِمِينَ ٦
Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.1
Footnotes
  • [1] Enyi mlio amini! Akikujieni mtu ambaye yuko nje ya sharia ya Mwenyezi Mungu akakupeni khabari yoyote, basi chungueni mjue ukweli wake, kwa kuchelea msije mkawaletea watu madhara, kwa kutojua hali yao. Hapo tena baada ya kwisha dhihiri kuwa hawana makosa mkaingia katika majuto ya daima, mkatamani yasingeli kuwa.