Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Qaf — Ayah 15

50:15
أَفَعَيِينَا بِٱلۡخَلۡقِ ٱلۡأَوَّلِۚ بَلۡ هُمۡ فِي لَبۡسٖ مِّنۡ خَلۡقٖ جَدِيدٖ ١٥
Kwani tulichoka kwa kuumba mara ya kwanza. Bali wao wamo katika shaka tu juu ya umbo jipya.1
Footnotes
  • [1] Kwani kutaka kwetu kulipungua, au uwezo wetu ulitetereka, hata tukashindwa kwa kule kuumba kwa mara ya kwanza, tusiweze tena kuwarejeza? Hasha! Hatukushindwa, nao wanatambua hayo. Bali wao wana shaka tu na wanadanganyikiwa na huku kuumbwa kupya baada ya kufa.