Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Qaf — Ayah 39

50:39
فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ ٱلۡغُرُوبِ ٣٩
Basi vumilia kwa hayo wasemayo, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi kabla ya kuchomoza jua na kabla ya kuchwa.1
Footnotes
  • [1] Ikiwa haya yamebainika, basi, ewe Mtume, yastahamilie hayo wayasemayo hao wanao kanusha, ya uwongo na uzushi kukhusu Utume wako. Nawe mtakasishe, Msabbih, Muumba wako na Mlezi wako na kila upungufu, ukimhimidi wakati wa alfajiri, na wakati wa alasiri, kwani ibada nyakati hizo ni jambo kuu.