Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah Al-Jumu'ah — Ayah 6

62:6
قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ هَادُوٓاْ إِن زَعَمۡتُمۡ أَنَّكُمۡ أَوۡلِيَآءُ لِلَّهِ مِن دُونِ ٱلنَّاسِ فَتَمَنَّوُاْ ٱلۡمَوۡتَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ٦
Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli.1
Footnotes
  • [1] Ewe Muhammad! Sema: Enyi nyinyi mlio Mayahudi! Kama mnadai kwa uwongo kwamba nyinyi peke yenu ati ndio vipenzi vya Mwenyezi Mungu, basi takeni mauti kwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli katika hayo madai ya kwamba Mwenyezi Mungu anakupendeni.