Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.1
Footnotes
[1]
Wanaafiki wanasema kwa kutoa ahadi: Tukirejea Madina hapana shaka kikundi chetu, ambacho ndicho chenye nguvu zaidi, kitakitoa kikundi cha Waumini ambao ni wanyonge! Nguvu anazo Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Waumini; sio hawa wanao jitia kuahidi. Lakini wanaafiki hawajui kitu.