Ali Muhsin Al-Barwani

Ayah by Ayah

Tags

Download Links

Ali Muhsin Al-Barwani translation for Surah At-Taghabun — Ayah 7

64:7
زَعَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَن لَّن يُبۡعَثُواْۚ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبۡعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلۡتُمۡۚ وَذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ ٧
Walio kufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyo yatenda. Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.1
Footnotes
  • [1] Makafiri wamedai kwa uwongo kwamba hawatafufuliwa baada ya kufa kwao. Ewe Muhammad! Waambie: Mambo sio kama mnavyo dai nyinyi. Ninaapa kwa Mola wangu Mlezi! Hapana shaka yoyote nyinyi mtafufuliwa baada ya kufa kwenu, na hapana shaka yoyote kuwa mtaambiwa mliyo yatenda duniani. Kisha mtalipwa kwayo. Na huko kufufuliwa, na kuhisabiwa, na kulipwa, ni jambo sahali na jepesi kabisa kwa Mwenyezi Mungu.